Mambo haya 10 yatakusaidia kuishi kwa amani.
Wakuu habari za wakati, nina imani tu wazima wa afya ila kwa wagonjwa Mungu awape tumaini. Leo Number ni 26 nimeona ni share nanyi kitu kidogo. Yafuatayo yatakusaidia wewe na mimi walau kidogo tukapunguza kuwa na "makasiriko" kati yetu na kufanya amani itawale:- 1. MUNGU. Kuna msemo unasema "God first", yes nadhani katika harakati zetu tukimuweka mbele Yeye basi kifuatacho ni AMANI 2. SAMEHE. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wengi wapate "jaka la moyo" ni kushindwa kusamehe. Hebu samehe sasa upate AMANI na afya 3. ISHI MAISHA YAKO. Yes hebu fanya kama una deal na mambo yako uone kama hutopata AMANI. Acha kufatilia ya watu utakufa 4. ONDOA MAWAZO HASI. Hebu acha hiyo dhana ya mtu akifanya kitu/jambo basi wewe ni kukosoa tu, hivi utapata AMANI kwa style hiyo? Mwisho utakuwa mchawi sasa 5. KUWA NA SHUKURANI. Vitu vidogo tu vinaweza kukupotezea AMANI moyoni, kumbe ukishukuru kwa vitu kama afya, pumzi, mazingira, kuamka salama, kupenda & kupendwa nk.....