Mambo haya 10 yatakusaidia kuishi kwa amani.
Wakuu habari za wakati, nina imani tu wazima wa afya ila kwa wagonjwa Mungu awape tumaini. Leo Number ni 26 nimeona ni share nanyi kitu kidogo.
Yafuatayo yatakusaidia wewe na mimi walau kidogo tukapunguza kuwa na "makasiriko" kati yetu na kufanya amani itawale:-
1. MUNGU. Kuna msemo unasema "God first", yes nadhani katika harakati zetu tukimuweka mbele Yeye basi kifuatacho ni AMANI
2. SAMEHE. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wengi wapate "jaka la moyo" ni kushindwa kusamehe. Hebu samehe sasa upate AMANI na afya
3. ISHI MAISHA YAKO. Yes hebu fanya kama una deal na mambo yako uone kama hutopata AMANI. Acha kufatilia ya watu utakufa
4. ONDOA MAWAZO HASI. Hebu acha hiyo dhana ya mtu akifanya kitu/jambo basi wewe ni kukosoa tu, hivi utapata AMANI kwa style hiyo? Mwisho utakuwa mchawi sasa
5. KUWA NA SHUKURANI. Vitu vidogo tu vinaweza kukupotezea AMANI moyoni, kumbe ukishukuru kwa vitu kama afya, pumzi, mazingira, kuamka salama, kupenda & kupendwa nk... Ni amani tosha
6. USITAFUTE UKAMILIFU. Amini kwamba ikiwa unatafuta eti ukamilike katika angle fulani ndio furaha yako ikamilike basi utasubiri sana! Na utakonda nakwambia!
7. FANYA UKIPENDACHO. Wenyewe wanasema "kitu roho inapenda", ndio fanya vile moyo wako unapenda na sio ufanye sababu ya fulani, utakufa!
8. KAA NA WATU SAHIHI. Hii itategemea na wewe mwenyewe, ukikaa na negative people basi utakuwa negative and vice-versa is true na utapata AMANI
9. PUMZIKA. Kuna watu wanakosa AMANI kwa sababu tu ya kushindwa kujipumzisha. Mtu muda wote upo busy eti "umechelewa" aisee! Hivi huo utulivu na nafsi na akili unapata wapi
10. JIPONGEZE. Letaa... Letaaa pombeee...,Hii ni tofauti kidogo na kupumzika maana unaweza kupumzika na ukakosa AMANI. Kuna watu ili wapate amani ya moyo basi lazima wapate burudani iwe music au pombe
Comments
Post a Comment