BoT: Mnaoshikilia Dola mziweke sokoni kwenye mfumo rasmi

 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa tahadhari kwa wale wote wanaoishikilia dola ya Marekani kuwa wapo hatarini kupata hasara kutokana na uamuzi huo wa kuficha pesa hizo wakitegemea kupata faida katika soko la fedha.



Akizungumza katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Gavana wa Benki Kuu Emmanuel Tutuba, amesema Tanzania inatekeleza mikakati ya kuimarisha upatikanaji wa dola hivyo kuendelea kushikilia pesa hizo kuna athari ya kupata hasara badala ya faida.



"Niwaombe wanaoshikilia dola mziweke sokoni
 katika mfumo ulio rasmi, tutawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kujihusisha na biashara haramu ya soko la fedha (black market)," amesema Tutuba

Comments

Popular posts from this blog

Ukitumia hii dawa yenye mchanganyiko wa mizizi sita, utavuta wateja kwenye biashara yako mpaka watu washangae

Mambo haya 10 yatakusaidia kuishi kwa amani.

Fahamu Kuhusu Kampuni za Mfukoni-Briefcase Corporations